MALENGO YETU

 • Kulinda na kuendeleza hadhi ya kazi ya uwalimu pamoja na kusimamia, maadili, maarifa na ujuzi kwa kiwango cha juu zaidi.
 • Kulinda, kusimamia na kuendeleza maslahi ya kazi ya uwalimu na kuwa kivutio kwa watu wengine kuipenda.
 • Kuwahimiza walimu kufanya kazi kwa bidii, na kuonyesha mfano wa utendaji kazi kwa uadilifu wa tabia na vitendo.
 • Kuhakikisha kuwa waajiri wanatambua umuhimu wa chama cha Walimu na walimu wana uhuru wa kujiunga na chama chao, na uhuru wa kufanya migomo inapobidi kufanya hivyo.
 • Kuhakikisha waajiri na walimu wanazingatia na kutekeleza sheria na kanuni za nchi zinazohusu kazi na mikataba ya kazi kimataifa iliyopo na haki inazingatiwa.
 • Kuwaelimisha wanachama masuala yanayohusu ajira zao pamoja na kuwapatia ushauri wa kisheria unapohitajika.
 • Kuhimiza na kuhakikisha kuwa walimu wanapata huduma zote wanazostahili kijamii, kiuchumi, na kiafya na kuwapa msaada kuunda vikundi mbali mbali vya kiuchumi katika kupambana na umaskini
 • Kujadili na kushauriana na waajiri juu ya wajibu, haki na mazingira bora ya kazi ya uwalimu na kufunga nao mikataba yao ya hiari.
 • Kuhakikisha kuwa katika sehemu zote za kazi mwalimu hapati bughudha au udhalilishaji wa kijinsia au wa kimaumbile na haki zinapatikana bila ya ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, itikadi ya kisiasa, au elimu.
 • Kuwaandaa walimu kuwa mstari wa mbele katika kupambana na magonjwa hatari ya kuambukiza, madawa ya kulevya, na uharibifu wa mazingira katika kulinda afya zao na wanafunzi wao na jamii kwa jumla.
 • Kuhakikisha kuwa walimu wanafaidika vya kutosha kutokana na mikataba ya kimataifa inayowahusu wafanyakazi na walimu.
 • Kushirikiana na Vyama vyengine vya Wafanyakazi Nchini na Nje ya Nchi na kujishirikisha na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi