HISTORIA YA CHAMA CHA WALIMU

Dhana ya kuanzisha Chama hatua ya awali

Chama cha walimu kilizaliwa baada ya kuanzishwa sheria mpya ya Vyama vya Wafanyakazi iliyopitishwa katika Baraza la Wawakilishi mwaka 2001. Sheria ilivitaka vyama vilivyokuwepo kabla ya sheria kujibadili ili viwe vyama vya Kizanzibar kwa kilichojuilikana kuwa suala la Vyama vya Wafanyakazi si la Muungano. Kwa upande wa Walimu wa Zanzibar hali ilikuwa tofauti kabisa kwa sababu hawakuwa na chama baada ya kusimamishwa kwa Chama cha Walimu cha Tanzania (CWT) mwaka 1996.
Viongozi watatu waliokuwa Baraza kuu la Taifa wa CWT Mw. Kassim Mussa Ali, Mw. Nassor Salum Shaame na Mw. Ali Nassor Moh'd wakiongozwa na Naibu Katibu mkuu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi wakati huo Mw.Talib Omar Mbwana. Viongozi hao kama kamati waliweza kuwahamasisha walimu wa Zanzibar juu ya uwelewa na haja ya kuwa na chama cha Walimu cha Zanzibar.

Kikosi kazi hicho kilijitolea na kuhamasisha walimu kwa kufanya mikutano mbali mbali Unguja hatimae kilituma mjumbe kupeleka habari ya uwepo wa haja ya kuanzisha Chama cha Walimu huko Pemba. Mjumbe huyo ambae ni Mw, Nassor Salum Shaame huko Pemba alionana na Mw. Rabia Nassor Majid na Mw. Juma Khatibu Faki. ili kuanzisha vuguvugu la uanzishwaji wa Chama cha walimu kwa upande wa Pemba..

Hatua ya pili

Kamati ndogo mbili ziliundwa hapo baadae moja Unguja na Moja Pemba zikijipa majukumu ya manne makubwa.


 • Kutengeneza rasimu ya katiba

 • Kutafuta wanachama hamsini (50), ishirini na tano (25)Unguja na ishirini na tano(25) Pemba).

 • Kuteua uongozi wa muda wa Chama watakaowakilisha kwenye Usajili.

 • Kutafuta njia ya kupata fedha kwa ajili ya usajili.

Kupata Usajili

Chama cha Walimu Zanzibar (Zanzibar Teachers Union- ZATU) kiliundwa na kusajiliwa rasmi tarehe 14 February 2002. Hati Nambari A.008, Viongozi wa muda wa ZATU waliokwenda kwenye Usajili ni:

 1. Rabia Nassor Majid (Mwenyekiti)

 2. Ahmed Fadhil Ramadhan (Makamo Mwenyekiti (Marehemu))

 3. Mussa Omar Tafurwa (Katibu)

 4. Safia Ali Rijal (Mweka hazina)

Uongozi wa muda

Uongozi huu wa muda ulipewa muda wa mwaka mmoja kutimiza majukumu yafuatayo;-

 • Kupata wanachama wapya

 • Kufungua matawi

 • Kufanya uchaguzi ngazi ya Tawi, Kanda na taifa

 • Kukitangaza chama.

Mkutano mkuu wa Kwanza

ZATU ilifanya mkutano mkuu wake wa kwanza wa kihistoria tarehe14 februari 2003 na kuchagua viongozi wake kama ifuatavyo:-

 1. Mw. Rabia Nassor majid (Mwenyekiti)

 2. Mw. Hamid rajab juma (Makamo mwenyekiti)

 3. Mw. Safia Ali Rijal (mweka hazina)

 4. Mw. Isha Bakar Ali (Mratibu wa wanawake).

Wajumbe wa kamati tendaji ya Taifa ya Mwanzo

 1. Mw. Mussa Juma Mzee Mjumbe.

 2. Mw. Asha Haroum Abdalla Mjumbe.

 3. Mw. Khamis Ameir Juma Mjumbe.

 4. Mw. Maymuna Elias barabara Mjumbe.

 5. Mw. Khamis Abdalla juma Mjumbe (Marehemu).

 6. Mw. Suleiman Khatib Suleiman Mjumbe.

Watendaji waliteuliwa na Baraza kuu kwa mujibu wa katiba

 1. Mw. Mussa Omar Tafurwa Katibu mkuu.

 2. Mw. Khamis Ameir Juma Naibu.

 3. Mw. Juma Khatibu Faki Katibu kanda Pba.

 4. Mw. Nassor S. Shaame Katibu kanda Unguja.

Siri ya mafanikio

Mafanikio haya makubwa yalifikiwa kwamsaada mkubwa wa vyama rafiki vikiwemo Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Chama cha Walimu Denmark (DLF) kupitia Shirikisho la Vyama vya Walimu Duniani (Education International EI)